April 10, 2015

SAAD KAWEMBA
Hali ya sintofahamu imetokea ndani ya Klabu ya Azam ambapo viongozi kadhaa wa timu hiyo juzi walivurugana hadharani na kutaka kutwangana makonde baada ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City, kwenye Uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.


Tafrani hiyo ilitokea baina ya Meneja wa Azam FC, Jemedali Said na Mkurugenzi wa Ufundi wa Azam FC, Saady Kawemba ambapo walitaka kupigana baada ya kutokea mabishano makali kati yao.
 
JEMEDARI...
Tukio hilo lilitokea ghafla baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1 ambapo inadaiwa walianza kuzozana juu ya matokeo na kubishana juu ya safari ya timu hiyo kwenda Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar.

Wasamaria wema na baadhi ya viongozi wengine wa Azam FC akiwemo Kocha Iddi Cheche walijaribu kuwatenganisha viongozi hao baada ya kuona hali mbaya huku wakiendelea kurushiana maneno.


Walipoulizwa juu ya suala hilo jana, Kawemba alisema alitoa maagizo lakini hayakufanyiwa kazi hivyo akaagiza mtu mwingine ayatekeleze, kuhusu kukwaruzana, alisema hayo ni mambo ya ndani ya klabu. Upande wa Jemedali alisema: “Ni jambo la kawaida kupishana katrika kazi lakini kila kitu kipo sawa.”

Baadhi ya mashabiki wengi walioshuhudia tukio hilo, walilalamika wakiamini haikuwa sahihi viongozi wa Azam FC nao kuzozana hadi kufikia kutaka kupigana tena mbele ya mashabiki wengi.

Baadhi walilaani na kusema tayari hata viongozi wa Azam FC wameanza tabia za viongozi wa klabu nyingine, hali inayowaondoa kwenye ile njia ya kuonekana wao ni mfano wa kuigwa kutokana na mfumo wa kampuni yao.

1 COMMENTS:

  1. Hiyo ni dalili ya Jahazi kuanza kuzama,na bado Simba watachukua nafasi ya pili na hao rambaramba watabaki wakiuza sura mjini tuu!Chezea mnyama wewe!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic