April 25, 2015

HIVI NDIVYO ALIVYOKUWA MASAU BWIRE JANA KWENYE UWANJA WA TAIFA WAKATI TIMU YAKE IKICHAPWA 5-0 NA YANGA KABLA YA KUANZA KUTOA HADITHI ZAKE....
Masau Bwire haishiwi hadithi, jana ametoa kali ya mwaka pale alipowageuzia ubao Yanga na kuwapa hadithi nzuri ya ya mvuvi na samaki.



Ilikuwa ni baada ya kikosi chake cha Ruvu Shooting kutwangwa kwa mabao 5-0 na Yanga ikiwa ni siku moja baada ya msemaji huyo kuiita timu yake kigingi.

Alitamba kwamba timu yake haiwezi kufungwa na kufanywa njia ya Yanga kwenda kuchukua ubingwa. Lakini baada ya kipigo, akawataka Yanga wasishangae.

"Mambo yanakwenda yanabadilika, ni kama mvuvi ambaye amejaribu kutupa nyavu zake, akivuta anakuta hakuna samaki, anarudia tena hapati samaki.

"Si kila siku ni Ijumaa, mambo yanabadilika. Ni kawaida kabisa, sasa msione ajabu na sisi bado tuko imara kabisa," alisema Bwire na kufanya kauli yake hiyo kuwa gumzo kwelikweli.

Hata hivyo, picha inamuonyesha akiwa kama mtu aliyechanganyikiwa wakati akishuhudia kipigo hicho kutoka kwa Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic