April 25, 2015


Yanga imeamua kumtaguliza mtu nchini Tunisia ili kuangalia mazingira kwa ajili ya kikosi chake.

 Katibu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, amesema timu yake imeshatuma mtu Tunisia kuweka mazingira vizuri ya mechi yake ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika, dhidi ya Etoile du Sahel.

“Kuna mtu tumempeleka Tunisia ili atuandalie mazingira mazuri ya kufikia timu na kikosi cha watu watakaokwenda kuhakikisha tunafanya vizuri,” alisema.


Wikiendi iliyopita, Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 na Etoile jijini Dar es Salaam, timu hizo zitarudiana wikiendi ijayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic