Waziri mkuu wa zamani wa
Italia, Silvio Berlusconi amekutana na bilionea wa Kithailand, Bee Taechaubol kujadili
suala la ununuzi wa klabu ya AC Milan.
Berlusconi ameimiliki AC
Milan kwa takribani miaka 30 lakini mashabiki wanaonekana kuchoka na sasa
wamekuwa wakiandamana.
Mashabiki wa AC Milan
wameandamana kwa staili ya aina yake huku wakikaa uwanjani na kuonyesha maneno
yanayosisitiza kwamba “Sasa imetosha”.
Wengi wanataka kiongozi
huyo aiuze klabu yake ili mtu mwingine atakayeinunua ifanye vizuri.
AC Milan imekuwa ikisuasua
bila ya mafanikio. Kabla ya hapo, Milan imekuwa moja ya klabu zenye uwezo
mkubwa na mafanikio tele.
0 COMMENTS:
Post a Comment