April 29, 2015



Man City si mabingwa wa England. Hii ni baada ya ushindi wa mabao 3-1 ilioupata Chelsea dhidi ya Leicester City, leo.

Ushindi huo umeiwezesha kufikisha pointi 80 wakati waliokuwa mabingwa watetezi, Man City wana pointi 67 na wakashinda mechi zao tatu zilizobaki watafikisha pointi 79.


Sasa Chelsea iliyobakiza mechi nne mkononi, inaendelea kushindana na Arsenal ambayo iwapo itashinda mechi zilizobaki itafikisha pointi 82.

Hivyo Chelsea inahitaji ushindi wa mechi moja tu kujihakikishia ubingwa.

Katika mechi ya leo, Leicester ndiyo waliotangulia kufunga bao katika dakika ya 45.


Lakini Chelsea wakasawazisha kupitia Didier Drogba katika dakika ya 47, John Terry akaongeza la pili kabla ya Ramirez kufunga la tatu kwa shuti kali baada ya kutengewa na Cesc Fabregas katika dakika ya 83.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic