Kocha msaidizi wa Yanga, Charles Boniface
Mkwasa amesema hawatalala hata kidogo na kuridhika wakiwa katika hatua za
mwisho kutwaa ubingwa.
Mkwasa amesema mwishoni mwa ligi ndiyo
kipindi kigumu zaidi, wanalijua hilo.
“Tunajua sasa kila kitu kinaongezeka ugumu.
Utaona sasa tunatakiwa kushinda kila mechi na kila timu pia inataka pointi
tatu.
“Ugumu unaongezeka kwa kuwa kila mmoja
anazitaka pointi tatu. Wako wanakwenda kuteremka daraja, wengine wanataka
ubingwa au nafasi ya pili.
“Hatuwezi kubweteka na sisi pia tunataka
kushinda na umuhimu umeongezeka zaidi,” alisema Mkwasa.
Yanga inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa pointi 49 na ainatakiwa kushinda mechi mbili tu ikiwemo ya kesho dhidi ya Ruvu Shooting ili kubeba ubingwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment