AL SIYABI (KUSHOTO) AKIWANOA MAKIPA PAMOJA NA KOCHA WA MAKIPA WA SIMBA (KULIA). |
Kocha wa makipa wa timu za taifa za Oman,
Haroon Al Siyabi amesema hakuna njia ya mkato kwa makipa wa Tanzania zaidi ya
kujifunza njia kisasa.
Al Siyabi ambaye alikuwa nchini kuwapa
mafunzo amesema soka limekuwa likibadilika haraka sana.
“Mambo yanakwenda haraka sana. Vitu
vinabadilika na lazima wakubali kujifunza,” alisema.
“Mbinu mpya zinazalishwa kila mara, hivyo
kama haujifunzi, unajikuta umebaki na mambo ya zamani na inakuwa si lahisi
kupambana na mbinu za kisasa.”
Al Siyabi pia ni mkufunzi wa Shirikisho la
Sola la Oman (Ofa), Shirikisho la Soka la Asia (AFC) na Shirikisho la Soka la Kimataifa
(Fifa).
Alikuwa nchi kwa siku kadhaa akiwanoa makipa
wa Simba baada ya uongozi wa Simba kupitia mjumbe wa kamati ya utendaji, Musley
Al Rawah kumualika nchini.
0 COMMENTS:
Post a Comment