April 7, 2015



Mshambuliaji nyota wa Stand United, Abasirim Chiedebere raia wa Nigeria amesema ana imani kubwa Stand United itabaki Ligi Kuu Bara na msimu ujao, itakuwa tishio.


Stand United iko katika nafasi ya 11 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ambayo ni 'danger'. Imejikusanyia pointi 24 baada ya kucheza mechi 19.

Chid raia wa Nigeria amesema kikosi cha Stand kutoka Shinyanga kimekuwa kikiimarika kila kukicha.

"Kweli mechi ni chache sana zimebaki. Lakini tunajituma sana kuhakikisha timu inabaki ligi kuu.

"Stand ni timu nzuri sana, ina vijana wengi na watu wana upendo. Lakini matatizo hayaishi kila sehemu, kwetu tunachukulia kama changamoto," alisema Chid ambaye aliwahi kukipiga Taswa FC inayomilikiwa na waandishi wa michezo.

Mnigeria huyo sasa amekuwa tishio na tegemeo la upachikaji mabao katika kikosi cha Stand United.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic