Uongozi wa kikosi cha Stand United umetamba
kwamba ulijua kiungo Haruna Chanongo atakuwa msaada kwao kama ambavyo amekuwa
akifanya.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Stand United, Muhibu
Kanu amesema waliamua kumuomba Chanongo ajiunge na kikosi chao akitokea Simba
kwa kuwa waling’amua uwezo wake.
“Chanongo ni mchezaji mzuri, utaona sasa
amekuwa msaada mkubwa kwetu kwa kushirikiana na wenzake.
“Sisi (Stand) tulijua atakuwa msaada mkubwa
kwetu, mmeona namna anavyofanya kazi yake vizuri na kwa ufasaha,” alisema.
Simba ilimtoa Chanongo kwa mkopo baada ya
kuonekana hana uelewano mzuri na uongozi.
Chanongo alikuwa kati ya wachezaji waliokuwa
wakishutumiwa kuihujumu Simba na mwisho akapelekwa kwa mkopo.
Lakini sasa amekuwa msaada mkubwa kwa Stand
United na jana aliibuka shujaa kwa kuifungia bao la ushindi dhidi ya Mtibwa
Sugar.
0 COMMENTS:
Post a Comment