Wakati mechi mbili za robo
fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zikipigwa, Kocha Jose Mourinho aliamua
kuzipotezea na kwenda kuangalia mechi ya vijana.
Mourinho akiwa na mwanaye
Jose Junior waliungana kuangalia mechi ya U21 kati ya Fulham dhidi ya DC Porto.
Wakati yeye anaangalia
mechi ya watoto, timu nne zilikuwa zikipambana kuwania kucheza nusu fainali ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mabingwa watetezi Real
Madrid walikuwa nyumbani kupambana na Atletico Madrid na kushinda kwa bao 1-0.
Juventus walikuwa ugenini
dhidi ya S Monaco na kupata sare ya 0-0, wakasonga mbele.
Chelsea ilishang’olewa
katika michuano hiyo hatua ya 16 bora, hivyo Mourinho hakutaka hata kuangalia
mechi hizo maana ni machungu tu. Aaah!
0 COMMENTS:
Post a Comment