KUMEKUWA NA TABIA YA WAAMUZI KUTAKA KUADHIBIWA NA WACHEZAJI. MFANO HII ILITOKEA MWANZA WAKATI WACHEZAJI WA POLISI TABORA WALIPOMPIGA NA KUMPIGA MWAMUZI |
Mwamuzi
Reston Liyali amenusurika kichapo mbele ya Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu,
baada ya kutoa maamuzi yenye utata katika mchezo wa Kombe la Mtemvu hatua ya
makundi uliozikutanisha UVCCM na Sandali.
Mchezo huo
uliopigwa Jumanne ya wiki hii kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar,
ulivunjika kipindi cha pili dakika ya 60 baada ya mwamuzi kukataa bao la UVCCM
mbele ya mbunge huyo ambaye anadhamini mashindano hayo, hali iliyosababisha
kuondolewa kwa taksi ya kukodi uwanjani hapo.
Mwamuzi huyo
amesema kuwa alilikataa bao la UVCCM kwa sababu tayari alishapiga filimbi ya
faulo ambayo ilitokana na kipa wa Sandali kuumizwa, hali iliyotafsiriwa kuwa ni
upendeleo ambapo wao waliamua kugomea mchezo na kusababisha fujo.
0 COMMENTS:
Post a Comment