Siku
chache baada ya beki wa Yanga, Mbuyu Twite kuvurugana na kocha wake, Hans van
Der Pluijm, uongozi wa timu hiyo, umemwambia mchezaji huyo kuwa yupo huru
kuondoka kama ataona inafaa kufanya hivyo.
Baada
ya mvurugano huo uliotokea kwenye mechi dhidi ya Stand United, Jumanne
iliyopita, Twite alisikika akisema bora aondoke yeye klabuni hapo kuliko
kuendelea kufanya kazi na kocha huyo.
Katibu
Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha amesema kuwa Twite hakupaswa kusema hivyo kwa sababu
yeye ni mchezaji mkongwe na ni profesheno, alipaswa kutulia na siyo kuanza
kujibishana na kocha.
“Makosa
yalikuwa ya kwake (Twite), Rajabu Zahir na kipa Dida (Deogratius Munishi). Kama
aliona kocha hakumtendea haki hakupaswa kumjibu mbele za watu ila kama anataka
kuondoka milango ipo wazi, kwani hakuna mtu yeyote aliye juu ya Yanga,” alisema
Tiboroha.
Mkataba
wa Twite kuitumikia Yanga unatarajiwa kumalizika hivi karibuni baada ya Ligi
Kuu Bara kumalizika msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment