Kocha kuu wa Yanga,
Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amemsifu kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Simon
Msuva kutokana na kuzifumania nyavu kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara
inayoendelea.
Msuva kwa sasa ndiye
kinara wa kuzifumania nyavu katika Ligi Kuu Bara kwa kuwa na mabao 11, huku
akimuacha kwa bao moja mshambuliaji wa Azam, Mrundi, Didier Kavumbagu, ambaye
alikuwa anawaongoza kwa muda mrefu.
Kiungo huyo akiwa
chini ya Pluijm, amefanikiwa kufunga mabao nane kwenye ligi kati ya 11 huku
matatu akiwa ameyafunga wakati timu hiyo ilipokuwa ikinolewa na Mbrazili,
Marcio Maximo ambaye alitimuliwa mwishoni mwa mwaka jana.
Endapo Msuva
atafanikiwa kuibuka mfungaji bora msimu huu, basi atakuwa ameibakiza nyumbani
tuzo ya ufungaji bora ambayo mara ya mwisho mzawa kuichukua ilikuwa ni msimu wa
2011/12 ilipochukuliwa na John Bocco wa Azam, huku kwa misimu miwili mfululizo
ikichukuliwa na wageni.
Pluijm amesema: “Tangu
niichukue Yanga nimemuona Msuva akifunga mabao mara kwa mara, ni vizuri kwani
huwa anafanyia kazi akiwa mazoezini na ndiyo maana akiwa uwanjani hupata
ujasiri na kufanya kile kinachotakiwa.
“Hakika ni mchezaji hatari sana, tena
mara nyingi anapolisogelea lango.”
0 COMMENTS:
Post a Comment