April 1, 2015

Timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro, imeapa kubeba pointi sita katika michezo yao miwili ya Ligi Kuu Bara ambapo wanatarajia kucheza leo Jumatano dhidi ya Kagera Sugar na Jumamosi watapambana na Stand United, michezo yote ikipigwa kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.


Mtibwa ambayo kwenye msimamo wa ligi kuu inashika nafasi ya saba baada ya kuwa na pointi 23, itakuwa na kibarua kigumu kuzikusanya pointi hizo sita huku ikiwa kwenye harakati za kutaka kumaliza ligi kwenye nafasi nne za juu.

Ofisa habari wa timu hiyo, Thobias Kifaru, alisema wameenda mkoani humo wakiwa na imani kuwa watarudi na pointi hizo kutokana na walivyojiandaa.

“Tumejiandaa kurudi na pointi zote kwani tumejiandaa vya kutosha kuhakikisha tunamaliza ligi tukiwa ndani ya nne bora, vijana wapo katika ari nzuri ya kuzichukua pointi hizo,” alisema Kifaru.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic