Uongozi wa Simba umefikia kwenye makubaliano na beki wake Hassan Kessy kupitia kwa meneja wake.
Kessy
alijiondoa katika kikosi cha Simba akishinikiza kulipwa haki zake kwa mujibu wa
mkataba ikiwemo shilingi milioni 5 za sehemu ya dau la usajili na nyumba ya
kuishi kama walivyokubaliana na uongozi alipojiunga nao Desemba, mwaka jana
akitokea Mtibwa Sugar.
Meneja
wa Kessy, Athuman Tippo ‘Zizzou’ amesema; “Jana (juzi Alhamisi) mchana viongozi
wa Simba walinipa fedha za kodi ya nyumba ya Kessy.
“Sasa
tupo katika mchakato wa kutafuta nyumba nzuri ya kuishi mchezaji wangu, ila
kuhusu zile fedha nyingine (milioni 5) wametuomba muda wa kumalizia na
tumewakubalia.”
Tippo
ambaye amewahi kuichezea Coastal Union ya Tanga, alisema uamuzi wa Kessy kujiondoa
katika kikosi cha Simba ulikuwa sahihi kwani alikuwa anadai haki yake ya
msingi.
Kessy
alithibitisha kupokea kiasi hicho cha fedha kutoka Simba kwa kusema; “Nilikuwa
Morogoro lakini sasa nipo Dar na fedha tumelipwa, hivyo natarajia kujiunga na
Simba mapema wiki ijayo.”
0 COMMENTS:
Post a Comment