April 10, 2015


 
Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imefuzu kucheza michuano ya All African.


Twiga Stars imefuzu licha ya kipigo cha mabao 3-2 lkutoka kwa Zambia, She Polopolo.
 
Ushindi wa mabao 4-2 ugenini Lusaka, Zambia ndiyo uliouikoa Twiga Stars kufuzu kwa jumla ya mabao 6-5.

Katika mechi hiyo iliyopigwa Taifa, Twiga Stars waliongoza kwa mabao 2-0 ya Asha Rashid na Mwanahamisi Sherua.
 
Lakini kipindi cha pili kikawa kigumu iliporuhusu mabao matatu na kulala kwa 3-0.

Makosa ya safu ya kiungo, beki na kipa Fatma Baba kuwa katika kiwango cha chini, kulichangia kuizorotesha Twiga leo.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic