Simba imeendeleza ushindi baada ya kuichapa
Ndanda FC kwa mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam, leo.
Simba ilionyesha kiwango cha juu katika
mchezo huo na kufanikiwa ushindi wa mabao hayo matatu.
Ilianza kalamu yake ya mabao kupitia kwa
Jonas Mkude katika dakika ya nane tu na bao hilo likawafanya Ndanda kuamka na
kushambulia kwa kasi.
Hata hivyo, Simba walionekana kutulia na
kupiga pasi za haraka na fupifupi na dakika ya 16 wakapata bao la pili
Ramadhani Sinagano ‘Messi’ baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa wa Ndanda,
Saleh Malande.
Said Ndemla akaongeza bao la tatu katika
dakika ya 32 baada ya kuunganisha krosi nzuri ya Ibrahim Ajibu.
Ajibu huyohuyo alishindwa kuifungia Simba
bao la nyongeza baada ya kukosa penalti iliyotolewa baada ya Emmanuel Okwi
kuangushwa katika eneo la hatari.
Kipindi cha pili kilionekana cha ushindani
mkubwa lakini bado Simba waliafanikiwa kulinda mabao yao matatu na Ndanda
kutoka hawana kitu.
0 COMMENTS:
Post a Comment