Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeilima barua Klabu ya Simba likitaka kuhakikisha inakutana
na nyota wa Yanga, Amissi Tambwe kwa ajili ya kumaliza tofauti zao.
Hatua
hiyo imekuja kutokana na Tambwe kuishtaki Simba kutokana na kutolipwa madai
yake ya kiasi cha dola 11,000 (zaidi ya Sh milioni 20), kama fidia ya kukatishwa
mkataba wake, kabla hajasaini Yanga siku hiyohiyo baada ya kuachwa.
Katibu wa Simba, Stephene Ally, alikiri kupokea barua
hiyo na kusema walikuwa wanamsubiria Tambwe arejee kutoka Zimbabwe alikokwenda
na klabu yake kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kumenyana na FC Platinum.
“Ni kweli tumepokea barua kutoka TFF
kutuambia tukae chini na Tambwe ili tuelewane kuhusu madai yake. Tumelikubali
hilo ila kwa sasa tunasubiri arudi kutoka Zimbabwe ili tuweze kuzungumza naye,”
alisema Ally.
Simba
imekuwa na rekodi mbaya ya kuvurugana na wachezaji wake kimaslahi, huku hivi
sasa ikiwa na mvutano na nyota wake, Hassan Kessy.
Tayari
TFF limetoa tahadhari kwa timu aina ya Simba, kwamba zinaweza kujikuta zikifungiwa
usajili kutokana na kuwepo kwa kesi za madai ya malipo.
0 COMMENTS:
Post a Comment