Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda leo
amekabidhiwa vifaa vya michezo kutoka kwa kampuni ya Tanzania Kwetu Nyumbani (TSN).
Kampuni hiyo maarufu kwa uuzaji bidhaa
mbalimbali yakiwemo mafuta ta petroli na dizeli, imetoa vifaa kupitia vinywaji vya
Chilly Willy na Smart Sports, vitakavyotumika kwenye mashindano yaliyoandaliwa
na Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni, yatakayojulikana kama Kinondoni Cup.
Vifaa alivyokabidhiwa ni jezi za mpira wa miguu
seti 60, jezi za netiboli 40, pamoja na mipira 100, vyote vikiwa na thamani ya
zaidi ya Milioni 50.
Akizungumza na waandishi wa habari, Makonda alisema kuwa
anazishukuru kampuni hiyo kwa kutoa vifaa hivyo ambavyo vitatumika kwenye
mashindano hayo yatakayoshirikisha timu kutoka kata zote 34 za wilaya hiyo.
“Hii ni dalili ya kuonyesha kuwa wemeniunga
mkono, hivyo ni lazima niwashukuru katika hili, kazi imebaki kwa timu
kujitokeza kushiriki.
“Katika mpira wa miguu wanaume tutachukua timu
mbili kutoka kila kata, netiboli timu moja katika soka la wanawake tunatarajia
kupata timu 18, na timu zote hizo zitapewa vifaa,” alisema Makonda.
Kwa upande wake mwakilishi wa TSN, Hamisi Tembo
alisema, “Tumeamua kumuunga mkono katika hili baada ya kuona jambo
alilolianzisha lina faida kwa vijana pamoja na taifa, tunaamini vifaa hivyo
vitasaidia kuyafanikisha mashindano haya.”
0 COMMENTS:
Post a Comment