Mwanachama wa Yanga ambaye ni mlezi wa Kundi la Yanga International Supporter
(YIS), Madaraka Marumbo, juzi
alimkabidhi viatu maalum nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambavyo
atavitumia kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Etoile du Sahel.
Cannavaro alikabidhiwa viatu hivyo mara baada
ya mchezo dhidi ya Polisi Moro juzi ingawa hakuweza kucheza kwenye mchezo huo
kutokana na kuandamwa na majeraha.
Kiongozi huyo alifunguka na kusema kuwa aliamua kutoa zawadi
hiyo kutokana na kuthamini mchango wa nahodha huyo kwenye timu hiyo.
“Niliamua kumpa zawadi hiyo kwa kutambua
mchango wake na nikiwa kama shabiki wake pamoja na timu kwa ujumla. Nafahamu wana
mchezo mkubwa mbele yao, hivyo wanatakiwa kujituma kwa bidii na kuweza
kuwashangaza Waarabu hata kama watakuwa ugenini,” alisema Marumbo.
0 COMMENTS:
Post a Comment