Unaweza kusema bora hata
wale wanaofanya vurugu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam zinapokutana Simba
na Yanga.
Mechi za watani zina mambo,
si kwamba tunawasapoti waendelee na vurugu lakini hizi zilizotokea jana kule Belgrade
mji mkuu wa Serbia zilikuwa hatari.
Watani Red Star Belgrade na
Partizan Belgrade walikuwa wanakutana, aisee ilikuwa ni hatari ile mbaya.
Pamoja na mechi kwisha kwa
sare ya 0-0 lakini Polisi walichapana na mashabiki ile mbaya.
Kwanza walianza mashabiki
wa timu hizo, Polisi walipoingilia, wao wakawavamia na kuanza kuwatandika
ilivyo.
Polisi waliokuwa kwenye
Uwanja wa Red Star waliopoona wanazidiwa wakaanza kurusha mabomu ya machozi.
Mwisho mashabiki zaidi ya
50 waliumia, 41 wakakamatwa na kutiwa nguvuni na askari 35 wakajeruhiwa.
PICHA ZINASIKITISHA,
TUNAWAOMBA RADHI LAKINI LENGO UONE ILIVYOKUWA.
0 COMMENTS:
Post a Comment