April 4, 2015


Mmoja wa viongozi wa wazee wa klabu ya Yanga, Ibrahim amelalamika kuugua kichwa ghafla akiwa mjini hapa kuiunga mkono Yanga iliyotua hapa kuivaa FC Platnum katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho baada ya ile ya jijini Dar, wageni kulambwa mabao 5-1.


Mzee Akilimali alianza kuumwa na kichwa baada ya kupanda basi maalum lililoandaliwa na klabu ya FC Platnum kwa ajili ya kuwabeba wachezaji.
BASI ALILOPANDA MZEE AKILIMALI...
Taarifa za awali zilieleza basi hilo lilipuliziwa dawa kwa lengo la kuwalevya wachezaji, hivyo dawa hizo zilimuathiri Mzee akilimali na mashabiki wengine ambao pia walilalama kuumwa vichwa.

Mzee huyo aliingia katika basi hilo akiandamana na mashabiki wengine pamoja na waandishi wa habari na kuwapisha wachezaji kupanda katika basi walilokwenda nalo uwanja wa ndege kuwapokea.

Mchezo ulikuwa hivi; Tayari viongozi wa Yanga waliotangulia mjini hapa walikodi basi ambalo lilikuwa linalindwa muda wote.

Hata baada ya kutua kwa Yanga, hawakupanda basi hilo badala yake wakapanda lile la mashabiki aina ya Toyota Coasta ‘Mayai’.

Mashabiki nao wakapanda katika basi lililoletwa uwanjani na uongozi wa FC Platnum kwa ajili ya kuipokea Yanga.
Dereva wa basi lililoletwa na Platnum alikuwa akilalama kwamba alitumwa kubeba wachezaji na si mashabiki. Lakini haikusaidia.




1 COMMENTS:

  1. Kwa mtindo huu, Africa tutaendelea kusindikiza dunia katika soka!! Hayatou na coy yake wamegota hawana jipya!! Lazima Africa ibadilike, leo hii waarabu wanatawala soka la Africa lakini wakienda WC wanakula vichapo vya mbwa mwizi maana kule fitina hakuna ni soka tu!! Al ahaly pamoja na mafanikio yao hawajawahi fanya lolote kwenye club bingwa ya dunia, wakati TP mazembe wameenda mara moja tu na mafanikio tuliyaona ilibaki kidogo wabebe ndoo!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic