Pamoja na kuwa wageni, mashabiki wa Yanga
wameiteka sehemu kubwa ya mji wa Bulawayo.
Mashabiki hao, wamekuwa wakionekana sehemu
mbalimbali wakiwa na nguo za njano na kijani, wakisubiri mechi ya Yanga dhidi
ya wenyeji wake Platnum.
Yanga ilishinda kwa mabao 5-1 katika mechi hiyo
ya Kombe la Shirikisho jijini Dar.
Mashabiki wa FC Platnum wamekuwa wakijiamini
kwamba watashinda zaidi ya mabao manne. Lakini muonekano wa kujiamini wa
mashabiki wa Yanga unaonekana kuwakatisha tamaa.
Baadhi ya mashabiki wa Yanga wamekuwa
wakikatisha maeneo mbalimbali huku wakisisitiza kwamba wamekuja kuwapa kipigo
Platnum kwa mara nyingine.
Tayari kikosi cha Yanga kimewasili mjini hapa
kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa katika eneo la migodi.









0 COMMENTS:
Post a Comment