April 30, 2015

MSUVA NA NGASSA WAKIWA MAZOEZINI MJINI SOUSSE, USIKU HUU.
Yanga wameonyesha kweli hawataki mchezo, kwani pamoja na safari ndefu ya zaidi ya saa 13, lakini bado wametua nchini Tunisia na kufanya mazoezi.
Wachezaji Yanga walipumzika kidogo tu na baada ya hapo walianza safari ya kwenda mazoezi.


Kikosi cha Yanhga kipo mjini Sousse, Tunisia kwa ajili ya kuivaa Etoile du Sahel katika mechi itakayopigwa Jumamosi.

Katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikishi, Yanga na Etoile zilitoka sare ya 1-1 jijini Dar es Salaam.

Inaonyesha ilikuwa ni lazima Yanga wafanye mazoezi usiku huu ili ikiwezekana kesho wafanye mazoezi kidogo au kupumzika kabisa.

Pia walilazimika kufanya mazoezi usiku ili kuendana na muda wa mchezo ambao watacheza saa 1 usiku za Tunisia na saa 3 Usiku nyumbani Tanzania.


Pamoja na mashabiki kuonekana wamekata tamaa, Yanga wamekuwa wakisisitiza kwamba watapambana hadi tone la mwisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic