Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe ametangaza rasmi kwamba ana uhakika
kiungo Simon Msuva atatua Simba.
HANS POPPE |
Hans Poppe amesema hana
hofu hata kidogo na ana uhakika Msuva atajiunga na Simba baada ya kumaliza
mkataba wake wa mwaka mmoja uliobaki.
“Amebakiza mwaka mmoja tu
na Yanga. Akimaliza basi anakuja Simba, nataka mniamini,” alisema Hans Poppe.
Msuva ndiye anaongoza kwa
ufungaji mabao katika Ligi Kuu Bara akiwa amepachika mabao 17 hadi sasa.
Simba tayari imeishaanza
kufanya michakato ya usajili kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake.
Mambo mengi yamekuwa
yakifanyika kwa siri lakini Hans Poppe ameamua kuweka wazi hilo kuhusiana na
Msuva.
Kuota mchana hakuvunji sheria yoyote. Madeni ya Tambwe, Kocha Loga, Chanogo bado mtu anamwota Msuva.
ReplyDelete