BANDA (KUSHOTO) AKIWA MAZOEZINI NA JOSEPH OWINO. |
Kiungo mkabaji wa Simba, Abdi Banda, ametamka kuwa hajielewi kutokana na kuumwa gonjwa
la ajabu ambalo yeye binafsi haelewi limetokana na nini kwa sababu madaktari
wamesema haumwi ugonjwa wowote wakati yeye anajua anaumwa.
Kiungo
huyo ambaye amekuwa nguzo katika kikosi cha Simba siku za hivi karibuni, juzi
Jumatano alilazimika kuwa mtazamaji wakati Simba iliposhuka dimbani kumenyana
na Mgambo JKT ya Tanga katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Banda
amesema, alifanyiwa vipimo hospitalini lakini majibu
yakaonyesha hana ugonjwa wowote, jambo ambalo linazidi kumuweka katika wakati
mgumu.
“Yaani
hata sijielewi, maana mimi naumwa lakini hospitali wanasema siumwi. Hali hiyo
imesababisha niwe nje ya uwanja na sijui nitarudi lini. Nilishindwa kukitumikia
kikosi changu katika mchezo uliopita kwa sababu hiyohiyo,” alisema Banda kwa
masikitiko.
Alipoulizwa
daktari wa Simba, Yasini Gembe juu ya ugonjwa huo alisema: “Muulize msemaji
ndiye atakupa jibu.” Alipopigiwa simu msemaji wao, Haji Manara alisema: “Nipo
njiani naenda mazoezini nitafute baadaye.”
Kocha: Viongozi Simba wanamvuruga Sserunkuma
NENDA HANS CLINIC IPO KINONDONI KWA MANYANYA,ILITOKEA KWANGU NIKAENDA HAPO BAADA YA KUAMBIWA NA WASAMARIA WEMA NA SASA NIMEPONA.
ReplyDelete