April 9, 2015


Zlatan Ibrahimovic amefanikiwa kufunga mabao zaidi ya mabao 100 katika kipindi cha miaka mitatu aliyokuwa na klabu yake ya Paris Saint-Germain.


PSG ndiyo klabu tajiri zaidi Ufaransa kwa sasa nay eye alifunga mabao matatu wakati wakiitandika Saint-Etienne kwa mabao 4-1 katika mechi ya Kombe la Urafansa na Muargentina Ezequiel Lavezzi akafunga la nne.


Mabao hayo ya Zlatan yanaendelea kuthibitisha yeye ni mmoja wa wachezaji bora kabisa waliowahi kucheza katika kikosi hicho.

Lakini kwangu kama Mtanzania naona ni sehemu ya kujifunza kwa Watanzania wengi kwamba Zlatan ameweza, bado kuna nafasi kwa wachezaji wanaochipukia au walioanza kucheza.

Zlatan aliishi maisha ya shida, mama yake akiwa anauza unga na baba yake akifanya kazi za kubangaiza.

Asili yake ni Yugoslavia lakini wazazi wake walihamia Sweden, wakati mwingine walikuwa wakibaguliwa kwa kuonekana ni asili ya nchi chokambaya.

Lakini leo ni shujaa wa taifa la Sweden na anategemewa. Yote hayo hayawezi kupatikana kwa ulahisi bila ya kujituma.

Kujituma pia bila ya kuwa na malengo hakuwezi kuwa na faida. Hivyo ni vitu vinavyotegemeana.

Nimekuwa nikisoma kitabu cha maisha ya Zlatan kinachojulikana kwa jina la “I am Zlatan” yaani “Mimi ni Zlatan”.

Ni kati ya vitabu bora kabisa na utaona kinavyoeleza Zlatan alikopita. Hata maisha yake yalivyokuwa magumu alipokuwa akiichezea Barcelona licha ya kuendelea kuonyesha uwezo.

Alikuwa na malengo, alipania kufikia anachotaka. Leo anaweza, hata wewe unaweza, ila lazima upambane na ikiwezekana si sahihi kuwaza mwisho wa ndoto yako kabla hata haujafikia robo.


Wachezaji wengi wa hapa nyumbani Tanzania wanaamini Yanga na Simba ndiyo mwisho wa ndoto ambalo si jambo sahihi. Huu ndiyo wakati mwafaka wa kumfuata Zlatan utimize ndoto zako, jiamini Mtanzania mwenzangu, inawezekana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic