Bao la Alvaro
Morata ndiyo lililoivusha Juventus hadi fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Morata alifunga
bao la kusawazisha dhidi ya Real Madrid na kutengeneza matokeo ya 1-1
yaliyoivusha Juventus.
Madrid ndiyo
klabu iliyomlea, klabu yake ya zamani ambayo msimu uliopita alikuwa katika
kikosi cha fainali kilichobeba kombe.
Sasa
amewapokonya Madrid na anakwenda kulipigania dhidi ya Barcelona.
Bao hilo
linaonyesha kiasi gani kipaji wakati mwingine kinavyoweza kuwa bora kuliko
fedha.
Angalia Madrid
yenye wachezaji ghali kama Gareth Bale, Cristiano Ronaldo, Karim Benzema, James
Rodrigues lakini walishindwa kuiokoa na Morata aliyekuwa mchezaji wa Madrid
anayetokea benchi, ameing’oa timu yake hiyo ya zamani kwa kipaji chake!
0 COMMENTS:
Post a Comment