Kocha wa Simba aliyemaliza mkataba, amesema anausubiri uongozi wa timu hiyo utoe jibu.
Goran Kopunovic amesema anasubiri uongozi wa Simba ufikie uamuzi wa tamati yake.
"Kama mwanzo nilivyokueleza, ninaendelea kusubiri watasemaje. Kama umesikia mimi ndiye nasubiriwa kutoa uamuzi, basi sawa.
"Nimezungumza na uongozi na kuwapa ofa yangu. Hapa ninachosubiri ni uongozi uniambie uko tayari au la, basi nitakuja kusaini mkataba," alisema Kopunovic ambaye ametua nyumbani kwake nchini Hungary.
Wakati yeye anasema anausubiri uongozi wa Simba utoe uamuzi kuhusiana na tamati yake, tayri Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ameishasema kuwa wameishatoa ofa kwa Mserbia huyo na wanamsubiri yeye atoe uamuzi wake.
Taarifa za awali zilileza kwamba Kopunovic alitaka kulipwa dola 50,000 (zaidi Sh milioni 100) kwa ajili ya fedha ya usajili, jambo ambalo Simba walilikataa.
Pia imeelezwa kwamba alitaka mshahara mkubwa ambao Simba waliona hawawezi kuulipa.
0 COMMENTS:
Post a Comment