May 9, 2015

RUVU SHOOTING
Timu za Ruvu Shooting na Polisi Moro, rasmi zimeteremka daraja.


Timu hizo zimetoka Ligi Kuu Bara hadi Ligi Daraja la Kwaza baada ya zote mbili kupoteza michezo yao leo.
 
POLISI MORO
Ruvu Shooting imepoteza mchezo wake kwa kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Stand United katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Wakati Polisi Moro nayo imedidimizwa mjini Mbeya baada ya kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City.

Kutokana na vipigo hivyo, Polisi imeshika mkia kwa kumaliza mechi zake 26 za ligi hiyo ikiwa na pointi 25 na Shooting ikafuatia ikiwa na 29 sawa na Mgambo lakini zikatofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic