![]() |
| NDANDA |
Ndanda imeepuka kuporomoka hadi daraja la kwanza baada ya
kuichapa Yanga kwa bao 1-0.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Nangwanda
mjini Mtwara, Yanga ndiyo walioshambulia mara nyingi zaidi.
Hata hivyo, Ndanda walionekana kucheza kwa umakini mkubwa na
ushindi huo wa bao moja, umewawezesha kufikisha pointi 31.
Pointi 31, zimeifanya Ndanda ishike nafasi ya ishike nafasi ya
tisa nyuma ya Ruvu JKT.
Yanga walisafiri kwenda Mtwara wakiwa mabingwa, pia wakiwa
wamepoteza mechi yao iliyopita dhidi ya Azam FC ambayo walilala kwa mabao 2-1.








0 COMMENTS:
Post a Comment