| TELELA |
Kiungo wa Azam, Frank Domayo ameshindwa kujizuia na kujikuta akimpongeza
Salum Telela wa Yanga kwa kusema jamaa anajua na ametoa mchango mkubwa katika
ubingwa wa Ligi Kuu Bara wa Wanajangwani msimu huu.
Domayo amesema: “Telela anajua sana, kwa siku
za hivi karibuni nimeona anacheza vizuri pale katikati na kama hatosumbuliwa
basi atafika mbali katika maisha yake ya soka.”
![]() |
| DOMAYO WAKATI AKIICHEZEA YANGA |
Jumatano iliyopita wawili hao walionyesha
ufundi wa hali ya juu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati timu zao
zilipopambna ambapo Azam ilishinda mabao 2-1.
Telela alionekana kumzidi maarifa Domayo kila
mara katika mchezo huo uliochezwa dakika zote kwenye mvua na uwanja kuharibika
sehemu ya kuchezea ‘pichi’.








0 COMMENTS:
Post a Comment