Leo ni mwisho! Simba inashuka dimbani kuivaa JKT Ruvu
kukamilisha ratiba ya Ligi Kuu Bara ikiwa imekosa nafasi ya pili, lakini nyota
wake Emmanuel Okwi amewapoza mashabiki wa timu hiyo na kuwaahidi mambo makubwa
msimu ujao.
Okwi amesema ana uhakika msimu ujao kikosi
chake kitajitahidi na kushika moja kati ya nafasi mbili za juu na kushiriki
michuano ya kimataifa.
“Mambo tu hayakwenda kama tulivyotarajia msimu
huu, tulijitahidi kadiri ya uwezo wetu ili angalau tupate nafasi ya pili lakini
ndiyo kama mlivyoona, wenzetu walikuwa wazuri zaidi.
“Nawaambia tu Wanasimba watulie ili msimu ujao
tufanye kazi yetu na tutapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa,”
alisema Okwi, raia wa Uganda.
Okwi alisema moja ya sababu za kutofanya vizuri
kwa kikosi chao ni kuwa na wachezaji wengi ambao hawakuwa na uzoefu wa Ligi Kuu
Bara, pia kutumia mifumo miwili ya makocha katika msimu mmoja ilikuwa tatizo.
Yanga ndiyo iliyotwaa ubingwa wa Bara na
itashiriki Ligi ya Mabingwa mwakani na Azam FC imeshika nafasi ya pili na
itacheza Kombe la Shirikisho Afrika.







0 COMMENTS:
Post a Comment