Mkongwe Ivo Mapunda wala hana papara ya usajili katika klabu
yake ya Simba kwani mabosi wake wamemuahidi kumuongezea mkataba ambao mwenyewe
anataka uwe wa miezi 18 tu.
Ivo, kipa mzoefu katika Ligi Kuu Bara, alitua
Simba msimu wa 2013/14 akiwa chaguo la kwanza kwa Kocha Zdravko Logarusic na wa
sasa Goran Kopunovic, mkataba wake unaisha Mei 20, mwaka huu.
Ivo, alisema bado hajasaini
mkataba wowote na timu hiyo kwani anawasubiri viongozi wake waliomhakikishia
kumsainisha siku yoyote kuanzia sasa.
“Kwa sasa nawasubiri viongozi wa Simba ambao
waliniahidi kuniongezea mkataba, nitasaini mkataba wa mwaka mmoja na miezi sita
tu. Unajua mimi ni mchezaji ninayejali maslahi sana, nadhani mkataba mfupi ni
mzuri katika kuongeza thamani yako kama mchezaji,” alisema Ivo.







0 COMMENTS:
Post a Comment