Kiungo nyota wa
Manchester United, Marouane Fellaini hatimaye ameamua kufunguka na kuelezea
alivyomwaga chozi baada ya kupata uhakika kocha David Moyes alikuwa ametimuliwa
kazi.
Fellaini raia
wa Ubelgiji mwenye asili ya Uarabuni, amesema alishindwa kujizua na kumwaga
chozi baada ya kugundua kocha huyo kweli alikuwa amefukuzwa kazi Aprili, mwaka
jana.
“Nimefanya kazi
miaka sita na Moyes, kwangu alikuwa kama mzazi na alinisaidia sana. Mimi ni
binadamu, sikuwa na ujanja namachozi yalimwagika.
“Unajua
nilisikia kwenye vyombo vya habari siku moja kabla lakini sikuwa na uhakika
kama ni kweli au la.
“Siku
iliyofuata nilipofika mazoezini nilikwenda kwenye mgahawa, baadaye nikamuona
Moyes akiwa amevaa suti na si suti (trak suti), nikajua ni kweli.
“Baadaye
alinifuata na kunichukua hadi ofisini kwake ambako kule alinieleza ukweli
kuhusiana na kuondoka kwake huku akinisisitiza huo ndiyo mpira ulivyo, nililia,”
anaeleza Fellaini.
Moyes ndiye
alimsajili Fellaini kutoka Everton ambayo aliifundisha kwa muda mrefu zaidi na
kumfanya kuwa kocha wa tatu kwa kudumu katika klabu moja kwa muda mwingi nchini
England baada ya Alex Ferguson na Manchester United na Arsene Wenger na
Arsenal.









0 COMMENTS:
Post a Comment