Kocha machachari, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’,
amefunguka kuwa yupo tayari kufundisha timu yoyote kati ya Coastal Union na
Mwadui FC kwa kuangalia dau atakalopatiwa na timu hizo mbili msimu ujao.
Julio alifanikiwa kuipandisha Mwadui ligi kuu
lakini baada ya hapo akaombwa kuiongezea nguvu Coastal Union kwa muda lakini
Wagosi hao wa Kaya wamenogewa naye na wanataka aendelee kuwa nao.
Julio amesema kwa upande wake yupo tayari
kufundisha timu yoyote kati ya Mwadui na Coastal kwa kuwa anaangalia maslahi
zaidi na si vinginevyo.
“Kwa sasa bado sijaamua nitakuwa wapi msimu
ujao kati ya timu yangu ya Mwadui na Coastal Union, lakini nitaangalia timu ambayo
itanipa maslahi mazuri, kwani kufundisha ndiyo kazi yangu,” alisema Mwadui.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Mwadui, Omary
Khatibu, alisema kuwa kwa upande wao wanamsubiri kocha huyo atoe maamuzi iwapo
ataendelea na timu hiyo au la kwa kuwa hadi sasa hawana kocha.
“Sisi tunamsubiri Julio ambaye tumekubaliana aje
huku baada ya wiki mbili kuanzia sasa, hivyo yeye ndiye atakayetoa mapendekezo
juu ya wachezaji atakaotaka kuwasjili msimu ujao.
“Lakini kwa ujumla wachezaji tutakaoendelea
nao ni wale walioipandisha timu na baadhi kutoka ligi kuu ambapo tumeshafanya
nao mazungumzo na mambo yakikamilika tutaweka wazi kila kitu.
“Kuhusu Julio, tunasubiri jibu lake kama
atataka kuendelea tutaendelea naye na kama akikataa, basi tutamuacha na
kutafuta kocha mwingine,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment