HIKI NDICHO KIKOSI CHA ETOILE WANACHOTAKIWA NGASSA NA TWITE |
Wachezaji wa Yanga sasa wameonekana kuwa lulu
kufuatia viwango walivyovionyesha katika michuano ya kimataifa ambapo timu za
Etoile du Sahel ya Tunisia, Platinum ya Zimbabwe na BDF ya Boswana zimevutiwa
na wachezaji watano wa timu hiyo.
NGASSA. |
Yanga iliondolewa katika michuano ya kimataifa
hivi karibuni dhidi ya Etoile du Sahel kwa jumla ya mabao 2-1 huku ikiwa
imeacha gumzo kwa wapinzani wao hao kutokana na kuonyesha ushindani wa hali ya
juu licha ya kutolewa mashindanoni.
Wachezaji ambao wamezitoa udenda timu hizo ni
Amissi Tambwe, Mbuyu Twite, Mrisho Ngassa, Haruna Niyonzima na Kpah Sherman.
Chanzo kutoka ndani ya Yanga kimeeleza kuwa, viongozi wa timu hizo waliwataarifu juu
ya kuwahitaji wachezaji hao kwa ajili ya kufanya biashara.
“Timu za Etoile, Platinum na BDF tulizokutana
nazo zimetoa ofa ya kuwahitaji wachezaji wetu kwa lengo la kuwanunua kutokana
na kuvikubali viwango vyao ambapo kila timu imetaja wachezaji wake inaowaona
wanafaa.
“Wachezaji waliotajwa na timu hizo ni Tambwe
ambaye timu mbili za Platinum na Etoile zimevutiwa naye, Mbuyu Twite, Niyonzima
na Ngassa ambao wote wanatakiwa na Etoile huku Sherman akitakiwa na BDF.
“Kwa upande wa uongozi wenyewe hawajakataa
wala kukubali ofa hizo ambapo waliwataka wasubiri hadi wamalize mechi zao za
kimataifa mbapo tayari wameshatolewa ikiwa ni pamoja na ligi kumalizika, hivyo
wakati wowote kuanzia sasa timu hizo zitaleta maombi rasmi ya kuwahitaji
wachezaji hao,” kilisema chanzo hicho.
0 COMMENTS:
Post a Comment