Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima amesema
bado anaendelea kuusikilizia uongozi wa Yanga huku akisubiri pia mipango yake
mingine.
Niyonzima raia wa Rwanda, amezungumza na
SALEHJEMBE na kusema kwamba taarifa zilizozagaa mitandaoni, zilikuwa ni uzushi
mtupu.
“Nimeona taarifa mitandaoni kuhusiana na
mimi kusajili Yanga sijui kwa shilingi milioni mia na ngapi.
“Nimeshangazwa sana, najiuliza hawa watu
wanaozusha mambo yanawasaidia nini. Kama nikisaini, wala haiwezi kuwa siri hata
kidogo.
“Lakini kwa sasa kwa kuwa sijasajili, kwa
nini watu wazushe na kufanya mambo yawe ya kudanganya na kulazimisha,” alisema
Niyonzima akionyesha kutopendezwa na taarifa hizo.
Mkataba wa Yanga na Niyonzima, unatarajia
kufikia tamati ndani ya siku 60.
Niyonzima ambaye alikuwa injini ya Yanga
amekuwa akisisitiza, ataendelea kusubiri huku akipa nafasi Yanga, lakini ofa
yake kutoka Uturuki pamoja na ile ya Afrika Kusini, pia anazipa nafasi.
0 COMMENTS:
Post a Comment