MAAMUZI YA
KAMATI YA RUFAA YA NIDHAMU
Baada ya mahojiano kati ya mrufani Dk Damas Daniel Ndumbaro na Wakili
wa TFF Nd Emmanuel Muga, pamoja na Wajumbe wa Kamati ya rufaa ya
nidhamu kuwahoji wote, Mrufani na Wakili wa TFF, Kamati ya rufaa ya nidhamu
ilichukua uamuzi ufuatao:-
1.
Hoja ya kwanza cha rufaa,
kwamba kamati ya nidhamu haikuwa na nguvu za kisheria kusikiliza shauri lake,
Kamati ya rufaa ya nidhamu baada kusikiliza hoja za pande zote mbili, kwa
uamuzi wa Wajumbe wote kwa maana ya kuwa zote nne za Wajjumbe wa kamati ya
rufaa ya nidhamu, ilitupilia mbali hoja hiyo na kuona kwamba kamati ilikuwa na
mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa kuwa mkata rufaa ni afisa wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kwa mujibu wa Katiba ya TFF ya 2013. Uamuzi
katika hoja hii uliamuliwa kwa kura 3 dhidi ya moja.
2.
Hoja ya pili inayosema kwamba
kamati ilikosea kisheria kwa kutompa muda wa kuleta utetezi wake wala vielelezo
vyovyote vile kwenye shauri lake.
Kamati ya rufaa ya Nidhamu kwenye Shauri hili, baada ya kufanya
maamuzi kwa kupiga kura, kura za Wajumbe watatu zilitupiliwa mbali hoja yake na
kura moja kati ya kura nne ilikubaliana na hoja yake kwa uamuzi huo, kamati ya
rufani ya nidhamu ilitupilia mbali hoja hiyo kwa uamuzi wa wingi wa kura kwa
maana ya kuwa tatu dhidi ya kura moja.
Sababu za kutupilia mbali hoja hizo ni kwamba mrufani alipata
wito wa kwenda kwenye shauri, na akawakilishwa na wakili wake ( Nestory Peter
Wandiba ) kwenye Shauri hilo.
Shauri liliposikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe
10/10.2014 shauri lilipangwa kusikilizwa tarehe 11/10/2014 Lakini siku hiyo ya
pili si wakili wala Dr Ndumbaro alifika kwenye shauri hilo kwa maana hiyo basi
shauri lililazimika kusilikizwa upande mmoja kwa mujibu wa kanuni za nidhamu za
TFF ibara ya 94 (3).
3.
Hoja ya tatu linalosema kwamba kamati ilikosea kusiliza shauri upande mmoja
bila ya mtuhumiwa kuwepo, ni kukiuka haki yake ya msingi ya kusikilizwa.
Kamati baada ya kusikiliza utetezi kutoka pande zote mbili
kamati ilifanya uamuzi kwa kupiga kura, na kura tatu (wajumbe watatu)
walitupilia mbali hoja hiyo, dhidi ya kura moja (mjumbe mmoja) aliyeikubali
hoja hiyo.
Sababu za kutupilia mbali hoja hiyo ni kutokana na ukweli kwamba
mrufani alipata wito wa kuhudhuria shauri hili na akamtuma wakili wake, lakini
mrufani alishindwa kuonyesha vielelezo vya kuonyesha kwamba angesafiri kwenda
nje ya nchi ili kamati ya nidhamu iweze kuahirisha shauri mpaka wakati ambao
angekuwa amerejea lakini hakufanya hivyo.
Hata hivyo kwa mujibu wa Ibara 144(2) (3) za kanuni ya nidhamu
za TFF, mrufani angeweza pia kuomba kamati ya nidhamu ibatilishe uamuzi
iliyoutoa dhidi yake ili aweze kusikilizwa utetezi wake pia hakufanya hivyo na
aliamua kukata rufaa.
4.
Hoja ya nne inayosema kwamba kamati ilikosea kisheria katika uchambuzi wa
ushahidi wa mlalamikaji na hatimaye kutoa uamuzi uliomtia hatiani.
Kamati ya rufani ya nidhamu ilisikiliza kwa umakini hoja za
pande zote mbili na kujiridhisha kwamba mrufani alifanya makosa kwa kutoa
taarifa isiyosahihi na kupotosha maamuzi ya TFF kinyume na kanuni ya 41 (6) ya
kanuni za ligi kuu ya Tanzania toleo la 2014 (4) na pia kushawishi, kupotosha
au kuzuia maamuzi/utekelezaji wa maamuzi ya TFF kinyume na kanuni ya 41(16) ya
kanuni za ligi kuu za Tanzania ya (2014).
Wakati wa kufanya maamuzi, wajumbe watatu(3) kwa maana ya kura
tatu zilitupilia mbali hoja hiyo, na kura moja, kwa maana ya mjumbe mmoja
alikubaliana na hoja hiyo. Kwa maana hiyo, kamati ya rufaa ya nidhamu ya TFF
imetupilia mbali hoja hiyo.
Kwa uamuzi huu kamati inadhibitisha uamuzi wa kamati ya nidhamu
iliyosomwa tarehe 13/10/2014, uamuzi huu umefikiwa baada ya wajumbe kupiga kura
na uamuzi kupitishwa kwa wingi wa kura za wajumbe watatu, dhidi ya mjumbe mmoja
wa kamati hii kwa hoja ya 2,3 na 4 na wajumbe wote 4 walikubaliana kutupiliwa
mbali hoja ya kwanza.
Kwa hiyo Dk Damas Ndumbaro ataendelea kutumikia adhabu yake kwa
kutojihusisha na shughuli yoyote ya Mpira wa Miguu (Soka) kwa kipindi cha miaka
saba.
Hata hivyo mrufani Dk Damas Ndumbaro anayohaki ndani ya siku 10
kuanzia leo tarehe 10/05/2015 ya kuomba marejeo ya uamuzi huu mbele ya kamati
ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF chini ya Ibara 142 ya kanuni za nidhamu za TFF ya
mwaka.
Kila upande utabeba gharama zake Hukumu inasomwa leo tarehe 10/05/2015/.
0 COMMENTS:
Post a Comment