Azam FC imefikiria kuhusu straika wake, Didier Kavumbagu
kutingisha kiberiti na kutaka kurudi Yanga, kisha ikasema wala hakuna shida
aende tu.
Siku kadhaa nyuma mabosi wa Yanga waliokuwa
katika harakati za kumshawishi Kavumbagu arejee kwenye kikosi chao ili
kuimarisha safu ya ushambuliaji na Azam ilikuwa kimya tu.
Kaimu Kocha wa Azam, George ‘Best’ Nsimbe
ametoa mkono wa baraka kwa mchezaji huyo kuangalia mbele zaidi kwa manufaa yake
endapo anadhani Yanga ni mahali sahihi kwake.
Nsimbe alisema: “Siwezi
kumkataza mchezaji kuondoka kama ameamua, lakini huyu ni mchezaji muhimu kwetu
na ningependa abaki.
“Nitajitahidi kumshauri abaki lakini kama
ataamua mwenyewe kuondoka, basi aende tu maana moyo wake utakuwa umependa
kufanya hivyo. Naamini wapo wanaoweza kucheza nafasi yake,” alisema kocha huyo
wa zamani wa KCCA ya Uganda.
Habari kutoka ndani ya Yanga zinasema uongozi
unafanya jitihada zote kuhakikisha Kavumbagu anasajiliwa kwani ni chaguo la
Kocha Hans van der Pluijm ambaye hana mshambuliaji wa uhakika katika kikosi
chake.







0 COMMENTS:
Post a Comment