Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amewatoa hofu mashabiki na
wanachama wa timu yake kwamba atasajili winga hatari kuziba pengo la Mrisho
Ngassa anayetimkia Free State Stars ya Afrika Kusini.
Ngassa ambaye mkataba wake umeisha siku chache
zilizopita, muda mrefu alikuwa ameshasaini kuichezea timu hiyo ya Afrika Kusini
na alibaki nchini kumalizia muda wa kuitumikia Yanga.
| PLUIJM |
Pluijm, raia wa Uholanzi amesema,
mashabiki wasiwe na hofu kuhusu kuondoka kwa Ngassa kwani hakuna ubaya wowote
kwa mchezaji kuondoka, isipokuwa wanatakiwa kumuombea maisha mema aendako.
“Sina hofu yoyote kuhusu kuondoka kwa Ngassa,
japokuwa ni mchezaji mwenye uwezo mzuri na unayeweza kumtegemea kikosini,
lakini hakuna jinsi, ni lazima aondoke, ingekuwa ngumu kumzuia.
“Mashabiki waondoe hofu kwani timu ndiyo
inaingia katika kipindi cha usajili ambacho tutasajili mchezaji kama Ngassa
uwanjani lakini huyo mpya atakuwa hatari zaidi,” alisema Pluijm.
Katika mchezo dhidi ya Azam FC katikati ya
wiki hii, Ngassa alitumia muda mwingi kuwaaga mashabiki wa Yanga baada ya
mchezo huo ambao Azam ilishinda mabao 2-1.







0 COMMENTS:
Post a Comment