Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal
Malinzi ametuma salaam za pole kwa wakazi wa Dar es salaam na hasa wale
walioathirika na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam kwa siku ya
tatu mfululizo sasa.
Katika salam zake kupitia kwa Mkuu wa Mkoa Dar es salaam, Mecky
Sadik, Malinzi amesema familia zimepoteza makazi, miundombinu ya usafiri na
michezo imeharibika na hata kuwa katika hali ya kutotumika, wanawake watoto,
familia, shughuli za kiuchumi na kimichezo zimeathirika na mvua hizi.
TFF inaunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa Dar es salaam, Serikali
na wadau wote wanaoshugulika kupunguza makali ya janga hili.








0 COMMENTS:
Post a Comment