Unaweza kusema miujiza, maana Coastal Union iliyokuwa ikipambana kuepuka kuteremka daraja, imemaliza Ligi Kuu Bara ikiwa katika nafasi ya tano.
Coastal Union imepanda hadi katika nafasi ya tano baada ya ushindi wake wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Coastal Union imeshinda mechi hiyo ikiwa ugenini na kufanikiwa kufikisha pointi 34 na kukaa katika nafasi hiyo ya tano.
Mbeya City imebaki katika nafasi ya nne, pia ikiwa na pointi 34 kama Coastal Union.







0 COMMENTS:
Post a Comment