Kocha Jose Mourinho wa
Chelsea anajulikana kwa utukutu. Lakini bado unaweza kumsifia kutokana na ubora
wa mambo mengine kwa kuwa mwelewa.
Wakati kiungo mkongwe na
gwiji wa Liverpool, Steven Gerrard alipotolewa katika mechi dhidi ya Chelsea,
Mourinho na mashabiki wa Chelsea walisimama na kumpigia makofi.
Mashabiki hao walimpigia
makofi Gerrard ikiwa ni kama kumuaga kwa kuwa ndiyo mechi yake ya mwisho akiwa
na Liverpool dhidi ya Chelsea kwenye Uwanja wa Stamford Brigdge.
Kumbuka, Gerrard wakati
anatoka, alikuwa ndiye aliyefunga bao la kusawazisha dhidi ya Chelsea na
matokeo yalikuwa 1-1 wakati huo, hadi mwisho wa mchezo.
Kuna kila sababu ya kuona
Mourinho ni muelewa kwa kuwa aliwaongoza mashabiki hao wa Chelsea kupiga makofi
hao ya pongezi.
0 COMMENTS:
Post a Comment