Masau Bwire amesema ataendelea kuwa msemaji wa Ruvu Shooting hata kama itateremka hadi daraja la nane.
Bwire amesema hataondoka katika nafasi hiyo kwa woga wa kukosekana Ligi Kuu Bara kwa kuwa imeporomoka hadi daraja la kwanza.
"Kwanza ningependa watu wajue Saleh, mimi nitaendelea kuwa msemaji wa Ruvu Shooting, hii ndiyo timu yangu.
"Hata kama itaporomoka hadi daraja la nane, nitaendelea kuwa hapa. Kwa sasa tunaendelea kupambana na dhuruma kubwa tuliyokutana nayo katika mechi dhidi ya Stand.
"Tunajua haki yetu itapatikana, ikishindikana tutajua mbele la kufanya," alisema Bwire akiendelea kuonyesha imani yake kwa timu hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment