Unamkumbuka yule mzee
aliibuka na kusema yeye ni mmliki wa klabu ya Yanga, sasa nyumba yake imewekewa
Bonge la X na inatakiwa ivunjwe.
Nyumba ya Juma Mwambelo
anayeshikilia hati za umiliki wa majengo mawili ya Yanga ya Jangwani na Twiga
ambayo ni makao makuu ya klabu hiyo na lile la Mtaa wa Mafia, nyumba hiyo
inaonekana haiko sehemu sahihi.
Manispaa ya Kinondoni ndiyo
imepiga X katika nyumba ya Mwambelo ambaye anaishi eneo la Tandale jijini Dar.
Mwenyewe Mwambelo aliiambia
SALEHJEMBE kwa X hiyo ni ya kitambo.
“Kama wakivunja watatulipa
kwa kuwa si kwamba tuko hapa nje ya utaratibu.
“Tunasubiri wafuate
taratibu, tunaamini mambo yatakwenda hivyo,” alisema.
Mwambelo anayejulikana kwa
msimamo, amekuwa akisisitiza yeye ndiye mmiliki halali wa klabu hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment