TAMBWE AKIWA NA MWANAYE |
Straika
nyota wa Yanga, Amissi Tambwe, ameondoka nchini jana kwenda kwao,
Burundi kwa ajili ya kuonana na familia yake ambayo hivi sasa ipo katika
wasiwasi mkubwa kutokana na vurugu za kisiasa zinazoendelea nchini humo.
Tambwe
amesema kuwa imembidi aende nchini humo ili aweze kuona ni jinsi gani
ataisaidia familia yake hiyo ambayo haina tena amani kama ilivyokuwa hapo
zamani.
“Sina
jinsi,
imenibidi niende ila ni matumaini yangu nitafika salama na kwa uwezo wa
Mwenyezi Mungu nitajipatia ujasili wa kuweza kuisaidia familia yangu.
“Nimekuwa
nikiwasiliana nayo kila wakati lakini hofu ndiyo jambo kubwa lililotawala nafsi
zao,
jambo ambalo pia hata mimi linaniumiza na zaidi kila ninapowaona Warundi
wanzangu wakikimbia kuja Tanzania kuomba msaada wa hifadhi.
“Ikiwezekana
naweza kuja nao ili niishi nao hapa (Tanzania) kwa amani, nawaomba ndugu zangu
wa Yanga na Watanzania wote waniombee nifike salama na niweze kuisaidia familia
yangu,” alisema Tambwe.
Machafuko
ya kisiasa nchini Burundi yanatokana na uamuzi wa rais wa nchi hiyo, Pierre
Nkurunzinza kutangaza kuwania nafasi ya kugombea urais ili aingie madarakani
kwa awamu ya tatu, jambo ambalo linapingwa vikali na wapinzani
wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment