Baada ya kufanikiwa kusalia katika Ligi Kuu Bara ukiwa ni msimu wake wa kwanza
kushiriki ligi hiyo, uongozi wa Stand United umejipanga kuhakikisha unatenga
shilingi milioni 350 ili kusajili wachezaji wa uhakika, lengo ni kuwa na kikosi
cha ushindani msimu ujao.
Stand
ilipanda msimu uliopita na imeweza kumaliza katika nafasi ya 10 ikiwa na pointi
31 na kujihakikishia kushiriki ligi hiyo msimu ujao.
Mkurugenzi
wa ufundi wa kikosi hicho, Muhibu Kanu, amesema kuwa msimu ujao lengo lao kubwa
ni kufanya vema tofauti na walivyomaliza msimu huu, ndiyo maana wametenga kiasi
kikubwa cha fedha ili kukisuka kikosi chao.
“Tumemaliza
nafasi ya kumi kutokana na ugeni wa ligi lakini msimu ujao tunajipanga kufanya
vizuri kwa kufanya usajili ambao utaifanya timu yetu kuwa na ushindani mkubwa
kwa kutenga kiasi cha shilingi milioni 350.
“Lengo
ni kupambana kufanya vizuri kama unavyofahamu timu zimeongezeka, hivyo
tunahitaji kuwa makini hasa upande wa usajili. Tayari tumeanza mazungumzo na
baadhi ya wachezaji wetu na hata wale ambao tulikuwa nao
tunazungumza
kuhakikisha tunaboresha mikataba na kuweza kuwaongezea,” alisema Kanu.
0 COMMENTS:
Post a Comment