TELELA |
Unajua sababu ya Yanga
kucheza soka la kuvutia licha ya kufungwa bao 1-0 na Etoile du Sahel? Ni kiungo
Salum Telela kwani ndiye aliyewavuruga katikati.
Katika mchezo wa kwanza
wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam, Telela hakucheza kwani alikuwa
majeruhi wa kifundo cha mguu lakini juzi Jumamosi alicheza na kuisumbua Etoile
du Sahel.
Kwa mujibu wa Kocha wa
Yanga, Hans van Der Pluijm, Telela ndiye aliyechangia kwa kiasi kikubwa
kuivurugia mambo mengi safu ya kiungo ya wapinzani wao.
“Ujue ndiyo kwanza anatokea
katika majeraha, tuliwashtukiza kwa kumtumia kwani walikuwa hawamjui kabisa,
hivyo hawakuwa na mpango wowote dhidi yake.
“Uliona jinsi tulivyowazidi
katika kumiliki mpira kwenye kiungo na hata kasi yetu ilikuwa nzuri,” alisema
Pluijm.
Kiungo wa Etoile du Sahel,
Franc Kom alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 42 baada ya kumchezea rafu Simon
Msuva na kuzidi kuidhoofisha safu yao ya kiungo.
Bao pekee la Etoile du
Sahel lilifungwa dakika ya 25 na Ammar Jemal kwa kichwa akimalizia krosi safi
ya Kom. Yanga inarejea jijini Dar es Salaam leo mchana.
0 COMMENTS:
Post a Comment