May 4, 2015


Kiungo Mbrazili aliyeshindwa kujiunga na Yanga katika dirisha dogo la usajili Desemba, mwaka jana, Emerson de Oliveira Roque, ameonekana kuwa bado anahitajika ndani ya kikosi hicho baada ya mashabiki wa Yanga kumuomba arudi.


Kiungo huyo ambaye alikuwa bado hajapewa mkataba na Yanga, alifanikiwa kuichezea mchezo mmoja tu wa Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba uliopigwa Desemba 13, mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na kumalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Yanga iliyokuwa ikinolewa na Wabrazili, Marcio Maximo na Leonardo Neiva, iliamua kuwaleta nchini Wabrazili wenzao, Andrey Coutinho, Geilson Santana ‘Jaja’ na Emerson ili kukiongezea nguvu kikosi hicho.

Yanga haikuweza kudumu na Wabrazili hao wote kwani baada ya mchezo wa Nani Mtani Jembe iliamua kuachana nao ambapo kabla ya hapo Jaja yeye alikuwa tayari ameshajiondoa kikosini mwenyewe huku Coutinho akibaki mpaka Yanga ilipotwaa ubingwa wa 25 wa Ligi Kuu Bara hivi karibuni.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic